Huduma Zetu

Wakala wa Forodha

Msingi mkuu wa biashara ya kimataifa ndani ya Alte ni uwakala wa forodha. Tunajivunia ujuzi usio na kifani katika kukuhudumia kwa kufuata kanuni na taratibu za forodha kwa urahisi na uhakika. Mawakala wetu wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha watahakikisha kuwa watu wa forodha wanakuruhusu kuchukua bidhaa zako kwa haraka, bila kuwepo na uchelewesahi wowote au adhabu. Tunafuatilia kwa karibu sheria zote za forodha na marekebisho yake, kukupa ushauri wa uhakika na kuhakikisha kuwa sheria, kanuni na taratibu zote za forodha zinafuatwa ipasavyo katika kila hatua. Mbinu zetu makini huondoa uwezekano wa bidhaa zako kushikiliwa forodhani na kuhakikisha kuwa biashara yako inafanyika kwa haraka na kwa usalama zaidi.

Usafirishaji wa Barabara

Huduma zetu za usafirishaji kwa njia ya barabara ni za kuaminika, zenye ufanisi na salama. Alte Logistics inatambua kuwa usafirishaji kwa nji ya barabara siyo tu kuondoa bidhaa toka sehemu moja kwenda nyingine; ila ni kutimiza ahadi zako na majukumu yako kwa wateja. Huduma zetu ni za kisasa, na zinaendeshwa na teknolojia ya kisasa kwa ajili ya kufuatilia mwendendo wa bishaa zako kwa umakini wa hali ya juu. Tunakupatia huduma kulingana na mahitaji na ratiba yako, na kuhakikisha bidhaa zako zinakufikia kwa wakati, na kila wakati.

 

Usafirishaji wa Baharini

Usafirishaji wa baharini (majini) unaofanywa na Alte Logistics unaunganisha mabara na kufungua fursa za biashara duniani kote. Tunashughulikia usafirishaji wa bidhaa zako baharini kwa umakini na uangalifu wa hali ya juu.

Usafirishaji wa Bidhaa za Thamani

Linapokuja swala la usafirishaji wa bidhaa za thamani kubwa, swala la usalama sio chaguo, ni lazima na muhimu sana. Alte Logistics tuna uzoefu mkubwa sana wa kusafirisha bidhaa zenye thamani kubwa, tunazingatia sana itifaki na ufuatiliaji wa kutumia teknolojia za kisasa masaa yote. Wataalamu wetu wa maswala ya kiusalama hutathmini hatari zinazoweza kujitokeza wakati wanasindikiza bidhaa zako za thamani, na kuhakikisha bidhaa zako zinafika salama mahali panapohitajika. Uamini utaalamu na umakini wetu katika ulinzi na usalama wa bidhaa zako zenye thamani kubwa.

Scroll to Top